Barnaba awapa somo wasanii

0
833

Glory Mlay

MSANII wa bongo fleva, Elias Barnaba ‘Barnaba’ amewataka wasanii wenzake kutengenisha ustaa na umaarufu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Barnaba alisema, kuna baadhi ya wasanii wanachanganya mambo hayo mawili jambo ambalo linasababisha kuchafua kazi zao.

Alisema baadhi yao wanafanya mambo machafu kwa kutumia sanaa ili wajizolee umaarufu, lakini sio kuboresha kazi zao wakawa mastaa.

“Sitaki kuwasema wanachachafua taswira ya sanaa, lakini wanajulikana, hivyo hakuna sababu ya kufanya mambo kama hayo ambayo hayawezi kuelimisha jamiii,” alisema.

Alisema ili msanii afikishe ujumbe kwa jamii sio lazima afanye mambo ya ajabu, ila kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya kwa jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here