Bares: Wachezaji wangu waliridhika mapema

0
851

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Abdallah Mohammed ‘Bares’, amesema wachezaji wake walirizika hali iliyofanya wawape nafasi wapinzani wao ya kusawazisha mabao.

JKT Tanzania juzi waliwabana Azam katika uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex, Dar es Salaam na kutoka sare ya mabao 2-2.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Bares alisema mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kwani walipambana ili wavune pointi tatu lakini bahati haikuwa upande wao.

“Lengo letu ilikuwa ilikuwa ni ushindi na ndio maana tulipata bao la mapema lakini wapinzani wetu walikuja kusawazisha hadi dakika 90 zinamalizika matokeo yakawa sare,” alisema.

Alisema kwa sasa amewapa mapumziko wachezaji wake, ambao baada ya hapo ataendelea na mazoezi ili wajiweke fiti zaidi.

Bares alisema mipango yao ni kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kwani iwapo watafanya makosa, yanaweza kuwagharimu baadaye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here