25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Barcelona wapata pigo kwa Jordi Alba

Barcelona, Hispania

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu nchini Hispania, Barcelona wataikosa huduma ya beki wake wa pembeni Jordi Alba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Napoli, mchezo ambao utapigwa wiki ijayo.

Mchezaji huyo amepata tatizo la goti la kulia mwishoni mwa wiki iliopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Getafe ambapo Barcelona ilifanikiwa kushinda mabao 2-1.

Mchezaji huyo hakuweza kumaliza mchezo huo baada ya kuumia katika dakika ya 17, hivyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa na kuikosa baadhi ya michezo ikiwa pamoja na ule wa Ligi Kuu wiki hii dhidi ya Eibar.

Kutokana na majeruhi ambayo ameyapata beki huyo, inasemekana kuwa anaweza kuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu, hivyo anaweza kuukosa na mchezo wa El Clasico dhidi ya wapinzani wao Real Madrid, mchezo utakaopigwa Machi 1, mwaka huu huku Barcelona wakiwa ugenini kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Msimu huu Barcelona wapo kwenye kipindi kigumu hasa kwa kuwakosa baadhi ya mastaa wa kikosi cha kwanza kutokana na kuwa majeruhi.

Miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa nje kwa kipindi kirefu kutokana na majeruhi ni pamoja na Ousmane Dembele ambaye amefanyiwa upasuaji wa nyama za paja wiki iliopita na atakuwa nje kwa kipindi cha miezi sita.

Mchezaji mwingine ni Luis Suarez ambaye na yeye atakuwa nje hadi mwisho wa msimu, hivyo safu ya ushambuliaji kuwa na wakati mgumu kwa kuwa wakati wa uhamisho wa Januari mwaka huu hawakufanya usajili wa kuongeza nguvu kikosini.

Kwenye msimamo wa Ligi nchini Hispania, Barcelona wanashika nafasi ya pili wakiwa na jumla ya pointi 52 sawa na vinara wa Ligi hiyo Real Madrid huku wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufungwa na kushinda.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles