25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Barcelona kumzuia Suarez kutua Atletico Madrid

KLABU ya Barcelona inajaribu kuzuia mshambuliaji wao, Luis Suarez kujiunga na Atletico Madrid ya kumsajili ili kuepuka kuwaongezea nguvu wapinzani wao hao katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu Hispania, maarufu kama La Liga.

Mshambuliaji huyo raia wa Uruguay huyupo katika mipango ya kocha mpya wa kikosi hicho, Ronald Koeman ambaye amemfungulia mlango wa kutokea Nou Camp ili kupunguza mzigo mkubwa wa mshahara wake.

Kituo cha redio cha Onda Cero cha nchini Hispania kiliiripoti kwamba Barcelona imeiongeza Atletico Madrid kwenye orodha ya klabu  ambazo hawawezi kuziuzia mchezaji.

Mbali na Atletico, vigogo wengine wa soka barani Ulaya kama wapinzani wao, Real Madrid, Manchester City na PSG nao wapo katika orodha hiyo.

Ingawa Barca wanataka kumuondoa Suarez , lakini inaonekana wana wasiwasi huenda akawafunga watakapokutana katika mchezo wa ligi, pia wanaogopa kumpoteza bure.

Hatua hiyo imeifanya Atletico kufikiria kufanya  uhamisho wa Edinson Cavani katika dirisha hili usajili wa majira ya joto barani Ulaya, ikiwa mpango wa kumnasa Suarez utakwama.

Cavani ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na  PSG  na amekuwa akihusishwa kuungana na kocha wa Atletico,Diego Simeone  katika misimu michache iliyopita. Suarez alikaribia kujiunga na wababe wa soka nchini Italia, Juventus, lakini dili lilikwama dakika za mwisho.

Mshambuliaji huyo aliwasili nchini Italia wiki iliyopita kushughulikia taratibu za kupata pasipoti ya Italia ili kukamilisha uhamisho huo bila mafanikio.

Baada ya kuikosa saini ya Suarez, Juve ipo katika hatuaza mwisho kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Alvaro Morata kwa mkopo.

Mpango wa Morata kwenda Juve ulionekana utasaidia kurahisisha uhamisho wa Suarez kutua Atletico ikiwa Barca itakubali kumuachia.

Ripoti ya Onda Cero inadai kwamba Suarez na Barcelona wamefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake, hivyo mchezaji huyo anaweza kuondoka Catalunya bure.

Imeripotiwa kwamba Simeone ana hamu kubwa ya kumpata Suarez ili kuongeza nguvu zinazohitajika kwa timu yake ya Atletico.

Ikiwa makubaliano hayo yatafikiwa, Suarez atasaini mkataba wa miaka miwili na kupokea mshahara wa Euro  milioni 8.3 kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles