Barca: Messi atabaki hapa milele, akitaka kuondoka poa

0
938

lionel-messiCATALUNYA, Hispania

RAIS wa Barcelona, Josep Bartomeu, amedai kuwa staa Lionel Messi ana mkataba wa milele klabuni hapo, lakini hawatomzuia kuondoka ikiwa atataka kufanya hivyo.

Licha ya mkataba wa sasa wa Messi kumalizika mwaka 2018, tayari uongozi wa Barca umeanza harakati za kuhakikisha anamwaga wino ili aendelee kubaki Catalunya.

Bartomeu amekuwa akihangaika kuona nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 anabaki kwenye kikosi cha mabingwa hao wa La Liga na Ulaya.

Bosi huyo amesema kuwa, ingawa wanamhitaji sana Muargentina huyo, lakini hawatakuwa na jinsi ikiwa ataamua kuwakacha.

“(Messi) ana miaka mingi hapa atakayoihitaji,” alisema Bartomeu alipokuwa akihojiwa na mtandao wa ESPN.

“Lionel Messi ni mchezaji bora kuwahi kutokea katika historia ya mchezo wa soka duniani na anacheza hapa.”

Rais huyo amedai kuwa wamejipanga kuanza mazungumzo ya kumpa mkataba mpya nyota huyo miezi ijayo, lakini amejitapa kuwa wana uhakika wa kumbakisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here