23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Baraza la UVCCM lamvua uongozi Mwenyekiti wake Wilaya ya Moshi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) limemvua Uongozi, Hussen Salehe aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya Moshi vijijini kwa utovu wa nidhamu .

Hatua hii imekuja baada ya Baraza hilo kupokea mapendekezo yaliyowasilishwa katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro na kujiridhisha kuwa Salehe hatoshi kuendelea kushika nafasi hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Mei 24, 2021, jijini Dodoma na Katibu wa Umoja wa Vijana wa (UVCCM), Raymond Mwangwala kwenye kikao cha Baraza hilo.

Akiongea kwenye kikao hicho Mwangwala amesema kuwa Baraza Kuu lilijiridhisha na Kamati ilijiridhisha na kuona kwamba kwa tuhuma zile na mapendekezo yaliyotolewa katika kikao halmashauri kuu ya Mkoa hivo limemvua uongozi.

“Hivyo naagiza Mkoa wa Kilimanjaro kutangaza nafasi ya mwenyeki wa uvccm, katika wilaya ya Moshi vijijini,”amesema.

Katika hatua nyingine Katibu huyo wa UVCCM ameishauri Serikali kuona haja ya kuangalia upya suala la huduma za vifurushi kwa kulichukulia kwa umakini ili kuokoa ajira kwa vijana waliojiajiri katika uchumi wa kidigitali.

“Kazi yetu kama chama kuishauri serikali ,vijana wetu wanaelekea kukosa ajira kutokana na gharama kubwa za bando,tunaiomba Serikali yetu tukufu kuona namna ya kuboresha changamoto ya huduma za vifurushi kupitia mitandao ya simu.

“Kwani uwepo wa gharama za juu katika manunuzi hukwamisha vijana kukua kiuchumi kutokana na wengi kufanya shughuli zao kupitia mitandao ya kijamii,”amesema.

Katika baraza hilo,UVCCM pia imeazimia kumuenzi hayati Dk. John Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania kwa kuyaendeleza yale yote mazuri aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake.

Pia wamempongeza Rais wa awamu ya Sita, Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuteuliwa kwa ushindi mnono huku akiwawataka vijana kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Samia pamoja na serikali yake.

“Tutamlinda,tutamtetea Rais wetu, iwe mvua au jua,pia kwa kuongeza juhudi katika kufanya kazi na uzalendo katika nchi yetu tunampongeza Sana,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles