22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Baraza la uongozi wa mpito kuundwa Sudan

KHARTOUM, SUDAN

VIONGOZI wa waandamanaji wametangaza kuunda Baraza la uongozi wa kiraia la mpito ambalo litawekwa hadharani rasmi kesho, likiwa na lengo la kulishinikiza Baraza la Kijeshi la nchi hiyo kukabidhi madaraka kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Al Jazeera, Baraza la Kijeshi lililochukua madaraka mara baada ya kung’olewa kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo, Omar al-Bashir, limekumbwa na shinikizo la kutakiwa kukabidhi madaraka ya kuongoza Sudan.

Chama cha wanataaluma cha Sudanese Professionals Association (SPA), ambacho kimekuwa mstari wa mbele kuwaongoza waandamanaji kupinga utawala wa Al Bashir, kimetoa taarifa ya kutaja majina ya viongozi watakaounda baraza la kiraia ili kuliondoa lile la kijeshi. Pia chama hicho kimewaalika wanadiplomasia mbalimbali.

Akizungumza na Shirika la Habari la AFP, Ahmed al-Rabia, kiongozi kivuli wa makundi ya chama cha madaktari, wahandisi na walimu, alisema: “Tunataka Baraza la Kiraia liongoze nchi. Baraza ambalo litakuwa na wawakilishi kutoka Jeshini na kuchukua nafasi ya baraza la sasa kuongoza Sudan.”

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SOAS cha London, Ahmed Adam amesema: “Baraza la Mpito ni rahisi kukabidhi madaraka kwa uongozi mwingine ndani ya nchi yoyote. Baraza kama hilo huwa halina mipango yoyote ya kisiasa, bali kutekeleza matakwa ya watu na kuondoka”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles