BARAZA LA MJI WETE LAPIGA MARUFUKU BIASHARA

0
558

Na JUMA SALMIN-WETEBARAZA la Mji Wete Kisiwani Pemba, limesema halitoruhusu uuzwaji wa biashara yoyote inayoweza kuleta madhara zikiwemo za maji, katika kipindi chote cha Sikukuu ya Idd El-Fitri kama njia ya kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Baraza hilo, Philipo Joseph Ntonda, alipokuwa akizungumza na MTANZANIA ambapo alisema biashara ambazo zinaweza kuleta madhara kwa binadamu hasa magonjwa ya mlipuko hazitoruhusiwa katika Mji wa Wete.

“Biashara zinatakiwa ziwe katika hali ya usafi, tutaruhusu biashara za vitu vikavu tu na juisi za kwenye chupa sio nyinginezo, kwani kipindi hiki ni hatari kwa afya ya binadamu,” alisema Ntonda
Mkurugenzi huyo aliwasihi wazazi kuwapeleka watoto wao na wakati wote wawe makini na biashara za barabarani ambazo ni hatari kwa afya.

“Watoto wanajinunulia tu vyakula, hawaangalii kwamba kipo katika hali gani, hivyo wazazi wachukue tahadhari kubwa,” alisema

Mkurugenzi huyo pia aliwataka wazazi kuwa makini katika kuandaa vyakula kwa kuimarisha usafi jambo ambalo litasaidia kuepuka maradhi ya milipuko ikiwemo Kipindupindu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here