25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Baraza la Madiwani Kasulu lasikitishwa na uvamizi hifadhi ya Wanyamapori Makere

Mwandishi wetu, Kasulu

Baraza la madiwani na Viongozi wa Halmashauri ya Kasulu Mkoa wa Kigoma pamoja wametembelea eneo la hifadhi ya Makere na eneo la wazi la ardhi oevu ambalo limevamiwa na Idadi kubwa ya wafugaji na wakulima.

Eneo la Ikolojia Moyowasi-Malagarasi ni muhimu Kwa maslahi ya Uhifadhi Duniani na Taifa kwani Kuna wanyama ambao hawapatikani sehemu nyingine Duniani.

Katika eneo hili linalopakana na Ziwa Tanganyika pia Kuna ndege aina ya Korongo Nyangumi ambao hawapatikani sehemu nyingine Duniani na Kuna makundi makubwa za Zohe statunga na Pofu.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Elia Charles Kagoma akiwa pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Joseph Rwiza wakizungumza baada ya kutembelea eneo Hilo Jana wameeleza kusikitishwa na uvamizi unaoendelea.

Kagoma alitaka hatua za haraka kuchukuliwa na Mamlaka husika kuweka mipaka eneo hilo kutenga eneo la hifadhi na eneo la vijiji ili iwe rahisi kuwaondoa wavamizi wote.

“Lazima kuwepo alama maalum kuzunguka eneo hili ambalo ni kitaku cha uwindaji ili kuhakikisha uvamizi unakomeshwa,”alisema

Kwa upande wake Rwiza alitaka kuwepo na ushirikiano wa kupambana na wanaojihusisha na vitendo vya ujangili katika eneo Hilo ambalo ni muhimu Kwa maslahi ya Taifa.

Akizungumza na viongozi hao wa halmashauri,Meneja wa kitalu cha uwindaji ncha Makere na eneo la wazi uvinza,Shadrack Kagoma amesema eneo hilo sasa kuna ujangili kutokana na uvamizi wa watu.

“Tuna wageni wa kimataifa wa uwindaji katika eneo hili lakini shida wakifika wanakuta kitalu chetu Kuna uvamizi wa Mifugo,kilimo na majangili,”amesema.

Amesema wavamizi wakiwepo kutoka nchi jirani wanaingia Mifugo eneo la hifadhi na kulima na baadhi wanaojihusisha na ujangili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles