MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Barakah Da Prince’, ameamua kurudisha fadhila kwa kujenga maktaba ya kisasa, katika shule ya msingi aliyowahi kusoma inayoitwa Pamba iliyopo mkoani Mwanza.
Barakah alisema atatoa sehemu ya fedha zake zinazotokana na kazi yake ya muziki kwa ajili ya ujenzi wa maktaba hiyo na pia atafanya marekebisho madogo madogo kwenye majengo ya shule hiyo.
“Nimepata mafanikio kwenye muziki japo si mengi lakini nilichonacho nitakipeleka kwenye Shule ya Msingi Pamba kwa ajili ya kujenga maktaba ili wadogo zangu wasipate tabu ya kusoma kama niliyoipata mimi,” alisema Barakah.
Barakah aliongeza kuwa kutoa ni sadaka hivyo mtu yeyote anaweza kufanya kitu kama hicho na siyo lazima awe msanii au mtu maarufu.