Baraka Da Prince atamani kufanya kazi na Kiba

0
928

 NA BEATRICE KAIZA 

MSANII wa muziki nchini, Baraka Andrew maarufu kwa jina la Baraka Da Prince, amesema bado anatamani kufanya kazi na Ali Kiba na kufanya hivyo itakuwa njia sahihi ya kuwaonyesha mashabiki zao kuwa wapo sawa. 

Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema tangu amejitoa lebo Rockstar bado hajakutana na Kiba. 

“Sijakutana na Ali Kiba tangu nimejitoa Rockstar, nikikutana na yeye leo sidhani kama nitakuwa na kitu kingine cha kuzungumza naye tofauti na kumwambia turudi studio tufanye kazi. 

“Nafikiri hii itakuwa njia sahihi kwa mashabiki zetu kuwa sisi tupo sawa na watu wenye maneno kuacha kuongea,” alisema Baraka Da Prince. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here