25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Barabara ya Landani- Kiwira yenye urefu wa Km 5 mbioni kuanza kujengwa Ileje

INa Denis Sinkonde, Songwe

MKANDARASI aliyepewa kazi ya kujenga barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 5 kwa gharama ya Sh bilioni 5.7 ya Kiwira-Landani wilayani Ileje mkoani Songwe atakakiwa kumaliza mradi huo ndani ya mwaka mmoja kama mkataba unavyoelekeza.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi akiwa na Mkandarasi wakati wa kukagua eneo la mradi huo.

Akimkabidhi mkandarasi atakayetekeleza mradi huo Machi 21, 2023 kutoka Kampuni ya IRA GENERAL ENTERPRISES COMPANY LIMITED kuu wa wilaya hiyo, Farida Mgomi amemtaka mkandarasi huyo kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa.

Mgomi amesema tayari Serikali imemlipa mkandarasi huyo asilimia 15 ya fedha ili kumwezesha kuanza kazi bila kisingizio cha kukosa fedha na matarajio ni kutaka adha ya mzunguko wa kilomita 38 upungue na kuanza kutumia barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 5.

“Kukamilika kwa barabara hii kutaongeza pato la halmasahuri na Taifa kwani uzalishaji utaongezeka mara dufu na wawekezaji wataongezeka,” amesema Mgomi..

Meneja wa TARURA Mkoa wa Songwe, Mhandisi Kilian Daudi Haule amesema maagizo yaliyotolewa ya kuwasimamia wakandarasi watayatekeleza ikiwa ni pamoja na kupokea changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi katika kipindi chote wakiwa wanatekeleza mradi.


Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi akitoa maelekezo kwa Mkandarasi.

Msimamisi wa mradi huo kutoka makao makuu TARURA, Benjamini Magese ameomba mkandarasi kuajili wananchi wa eneo husika ambao ndio walindi wa mradi huo, ikiwa ni pamoja na kuonyesha ushirikiano ili mradi uende kwa kasi.

“Mkandarasi amekamilisha taratibu za kimkata na leo hii tunamkabidhi mradi tayari kwa kuanza, na tunampa siku saba za maandalizi tunatarajia Machi 28, 2023 mkandarasi awepo eneo la mradi tayari kwa kuanza kazi,” amesema Magese.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ubatizo Songa amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutasaidia kuongeza pato la halmashauri kutoka Sh 1,000 kwa tripu moja mpaka Sh 3,000 hivyo kumtaka mkandarasi ajikite kufuata yaliyopo kwenye mkataba.

Shughuli ya kujenga barabara hiyo yenye urefu wa km 5 inaanzia Landani yanapochimbwa makaa ya mawe hadi Kapeta mgodini yanapochakatwa kimadaraja na kupimwa uzito itaenda sambamba na ujenzi wa daraja kwenye mto Mwalisi lenye urefu wa mita 40 na kuacha kuzunguka Kyela urefu wa km 38.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles