23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Barabara mbovu aliyopita JPM yaondoa mameneja Tanroads

Na WALTER MGULUCHUMA-KATAVI

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,  Mwandisi  Isack  Kamwele  ametegua   uteuzi  wa maneja wawili wa mikoa ya Lindi na Pwani kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi ya kusimamia miundo mbinu ya barabara kwenye mikoa yao .

Kamwele alichukua uamuzi huo juzi akiwa njiani kutoka  Inyonga kwenda Mkoani Lindi wakati akikagua barabara inayojengwa kwa kiwango cha rami yenye urefu wa kilometa 1.6 inayotoka Kibaoni kwenda makao makuu ya Halmashauri ya Mpimbwe  Wilayani Mlele Mkoani Katavi 

Aliwataja  mameneja aliowasimamisha kazi kuwa ni Mwandisi  Isack Mwanawima  ambae  ni Meneja wa Tanroads wa  Mkoa wa Lindi na  Yudas  Msangi  ambae  ni Kaimu  Meneja wa Tanroads wa Mkoa wa Pwani .

Maagizo hayo ya kuwasimamisha kazi aliyatowa ikiwa ni siku moja baada ya  Rais Dk.  John Magufuli  kuonekana kutoridhishwa na  hali ya barabara za mikoa hiyo.

Rais Magufuli alitumia barabara hizo wakati akitokea mkoani  Mtwara kwenye  mazishi ya Rais wa Awamu ya Tatu,  Benjamini Mkapa.

Kamwele alisema Rais alipita kwenye barabara  ya  Miginyo  hadi Lindi  amekuta  barabara ya lami  lmeharibika sana imekuwa kama  barabara ya vumbi wakati fedha za matengenezo zipo.

“Pia  hata barabara hiyo inayopitia kwenye Mkoa wa Pwani nayo imeharibika hivyo kwa mamlaka niliyopewa na  Rais, mameja wa mikoa hiyo yote miwili anawasimamisha kazi.

Katika hilo alisema ni jambo la aibu kuona barabara zinaharibika na Rais aliyepita kuziona wakati na mameja hao wapo.

Alisema jambo hilo ni la aibu hata kwake na halijamfurahisha na ndio maana ameamua kuchukua uamuzi huo.

Mwandisi Kamwele alisema  Tanroads walikuwa na sifa nzuri  lakini wameanza kuharibiwa na watumishi wachache.

“Kwa hiyo watambue kuwa kipindi hiki sio cha  kufanya mchezo kila  anae bainika kushindwa kutekeleza wajukumu yake atambue kuwa atawajibishwa,” .

Aliwaagiza mameja wa Tanroads kuhakikisha ifikapo Agosti 30 mwaka huu barabaara zote ambazo ziliharibiwa na mvua za msimu huu matengenezo yake yawe yamekamilika.

“Wizara ya ujenzi imeishatoa kiasi cha shilingi bilioni 35 kwa ajili ya matengenezo ya barabara hizo kwa meneja atakaeshindwa kukamilisha matengenezo hayo ajue kuwa kazi yake ya umeneja ndio mwisho wake siku hiyo ya agosti 30,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles