30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bank ya CRDB yang’ara COP27 katika kutoa mchango kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

BENKI ya CRDB imekuwa benki pekee barani Afrika kupata fedha dola milioni 100 kutoka Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Green Fund kwa ajili ya kusaidia kukabiliwa mabadiliko ya tabia nchi kilimo.

Kwa mujibu wa CRDB fedha hizo zitawawezesha wakulima wa Tanzania kupata mikopo ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanaathiri uzaliwashaji wa chakula.

Meneja Mwandamizi wa Miradi Endelevu ambayo ni Rafiki kwa Mazingira kutoka CRDB, Kenneth Kasigila.

Meneja Mwandamizi wa Miradi Endelevu ambayo ni Rafiki kwa Mazingira kutoka CRDB, Kenneth Kasigila, akiwasilisha mada katika mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi(COP27) nchini Misri, anasema kuwa benki hiyo imekuwa kinara barani Afrika baada ya kuja na ubunifu wa mradi ambao ni wa kipekee.

“Tumehudhuria mkutano nchini Misri ili kushiriki na wanaharakati mbalimbali wa mazingira duniani kwa ajili ya kuunganisha nguvu zetu kuweza kupambana mabadiliko ya tabianchi.

“CRDB tumeanza siku nyingi kujihusisha na shughuli mbalimbali ambazo ni rafiki wa mazingira na vilevile kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na hata ukiangalia sera yetu ya benki moja ya misingi yake ni mazingira, na ndiyo sababu tumekuwa tukitoa ufadhili mbalimbali katika shughuli zinazohusiana na mazingira.

“Pia, mwaka 2019 benki yetu iliweza kusajiliwa na taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Green Fund ambapo katika Bara la Afrika kuna benki nne tu za kibiashara ambazo zimesajiliwa na taasisi hii.

“Lakini CRDB ndiyo benki pekee ambayo mradi wake wa dola milioni 100 umeweza kukubaliwa na kupata mkopo wa dola milioni 100 nyingine na hivyo kufanya mradi huu mzima ambao utajikita katika kuondoa changamoto mbalimbali za mabadiliko ya tabianchi zinazohusika na kilimo thamani ya dola milioni 200 zaidi ya Sh bilioni 460,” amesema Kasigila.

Kwa mujibu wa Kasigila mpango huo unawawezesha wakulima wadogowadogo ambao ndio wazalishaji wakubwa wa chakula wakabiliane na mabadiliko ya hali hewa kwa kupata mikopo, dhamana na bima kwa ajili ya mazao yao.

“Mradi huu umejikita zaidi katika kuwasaidia wakulima wadogowadogo ambao ndiyo wanaoendeesha shughuli za kiuchumi za nchi yetu na kama tunavyofahamu kwamba kilimo ni moja kati ya nyanja muhimu ambayo imeajiri wakulima wengi wengi nchini Tanzania, watu wengi ambao wanajishughulisha na kilimo ni wale mbao ni wakulima wa hali ya chini wanaokabiliana na changamoto mbalimbali za mabadiliko ya tabianchi,” amesema Kasigila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles