Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
KOCHA wa Simba leo Desemba 10,2021 ameshindwa kuzungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Yanga kutokana na bando la wadhamini lililowekwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mkutanoni hapo kuwa na nembo ya GSM.
Katika mkutano huo uliofanyika leo saa 11:00 asubuhi kwenye ukumbi wa TFF, jijini Dar es Salaam, uongozi wa Simba kupitia Kaimu Ofisa Habari klabu hiyo, Ally Shantri, waligoma kuingia mkutanoni licha ya Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo kuwataka waingie ndani.
Moja ya kauli ambayo Shantri alisikika akitoa baada ya kugoma alisemma bango la GSM litolewe kwanza.
Kutokana na Simba kugoma, aliyezungumza katika mkutano huo ni Kocha Mkuu wa Yanga,Nassredine Nabi, huku kocha wa Simba, Pablo Franco akizungumza kupiti mtandao wa klabu saa 7:00 mchana.
Mchezo huo unaoikutanisha miamba ya Kariakoo, utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, huku makocha wote kwa nyakati tofauti wakisema ni mechi ngumu.
“Mecho hautakuwa rahisi lakini nashukuru maandalizi yote yamekwenda vizuri, wachezaji wamekaa pamoja na kuelekeza akili zao zote katika mechi kwa kuepuka mambo ya mitandao,” amesema Nabi.
Kwa upande wa kocha wa Simba, Franco amesema”Ilatakuwa mechi ngumu, lazima tukubali hilo.Tutakwenda kupambana kwa ajili ya mashabiki wetu na kuwapa pointi tatu,”