25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

BANDARI YA TANGA HATARINI KUTOWEKA

Na AMINA OMARI- TANGA


BANDARI ya Tanga ipo hatarini kutoweka kama hatua za haraka za kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi zinazoendelea kwa sasa katika Kisiwa cha Toten kinachoendelea kuharibiwa na maji ya bahari, hazitachukuliwa.

Hayo yamesemwa jana na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Donald Ngaile, wakati wa ziara ya Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, alipotembelea Kisiwa cha Toten jana ili kujionea athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alisema kisiwa hicho ndilo eneo ambalo miundombinu ya kuongozea meli zinapoingia katika eneo la Bandari ya Tanga, ilipowekwa na kwamba kumomonyoka kwa kisiwa hicho, kunatishia uhai wa bandari hiyo.

“Kisiwa hicho ndiyo usalama wa bandari ulipo, lakini kasi ya mmonyoko inatishia kwa kiasi kikubwa usalama wa bandari.

“Kwa hiyo, tunaiomba Serikali iangalie hatua za haraka za kunusuru hali hiyo,” alishauri Ngaile.

Kwa upande wake, Kaimu Mhifadhi Mfawidhi wa Hifadhi ya Bandari ya Tanga, January Ndagala, alisema tayari kuna hatua za kuhifadhi kisiwa ambazo wameshaanza kuzichukua.

“Tumejipanga kufanya tathmini ya kina kwa kushirikiana na Jiji la Tanga pamoja na Bandari ili kuweza kuja na namna bora ya kudhibiti mmomonyoko wa ardhi kisiwani hapo,” alisema Ndagala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles