26.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

Bandari ya Nyamirembe kubeba mizigo nchi za nje

MWANDISHI WETU-CHATO

Hatua ya Mamlaka ya Usimami Iwa Bandari Tanzania (TPA), kukamilisha ujenzi wa Bandari ya Nyamirembe Wilayani Chato mkoani Geita, sasa kutafungua milango ya usafirishaji wa mzigo na shughuli za utalii nchini.

Pamoja na hilo pia Bandari hiyo, itakuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo katika nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuanzia Machi mwaka 2020.

Akizungumza leo wakati wa ziara ya kutembelea miradi inayotelezwa na TPA, Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Morris Machindiuza, amesema kuwa Bandari ya Nyamirembe ni lago muhimu kwa uchumi wa Ziwa Victoria kwani kwa muda mrefu imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa maeneo hayo na wasafirishaji wa mizigo.

“Nyamirembe ni Bandari muhimu sana kwetu TPA, kihistoria ilianza kufanyakazi mwaka 1960 na ilipofika mwaka 1967 tangu wakati huo ilikuwa chini ya Shirika la Reli Tanzania lakini kutokana na mabadiliko ilipofika mwaka 1997 ilikabidhiwa kwa Kampuni ya Meli.

Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Morris Machindiuza

“Tangu wakati huo zipo meli zilikuwa zikifika hapa na kutia nanga na ambayo ilikuwa na uwezo wa kuibeba abiria 593 na kuibeba tani 350.

“Na meli hii ilikuwa ikibeba mazao mbalimbali yakiwamo ya pamba, mchele na ilikuwa kama daladala katika maeneo yote muhimu. Na sasa TPA kutokana na umuhimu wake tuliwekeza na kuiuhisha kwa kuanza ukarabati wake kwa gharama za za Shilingi bilioni 4.128 ikiwamo ujenzi wa gati, jengo la abiria, mnara wa meli.

“Na hii bandari sasa itakwenda kuchochea utalii kwani hapa imepakana na Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato, Rubondo ambapo pia shughuli za utalii zitaongezeka. Kwanza kusafiri kwa maji ni utalii mkubwa na pia wapo ambao hupenda kuanza kwenye Hifadhi na kisha kutafuta kumpumzika kwenye maeneo ya fukwe ikiwamo kusafiri kwa meli,” alisema Mchindiuza

Bandari ya Lushamba

Machindiuza, alisema kuwa TPA  imedhamiria kuimarisha bandari zote katika Kanda ya katika Ziwa Victoria  ikiwamo kuhakikiisha inajenga miundombinu pia katika Bandari ya Lushamba katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema ujenzi ambao umetumia ambao umetumia Sh bilioni 1.265 umekamilika na hivyo huduma rasmi katika bandari hiyo unatarajia kuanza mwezi huu.

Alisema kabla ya kukamilika kwa ujenzi wa bandari la Lushamba usalama wa abiria na mzigo yao hakuwa salama kwani walikuwa wakilazimika kabla kuingia kwenye chombo kuanza kupita kwenye maji hali iliyokuwa changamoto hasa kwa wagonjwa ambao hawakuwa na uwezo kabisa wa kupita ndani ya maji.

“Mradi huu wa ujenzi wa gati la Lushamba rasmi ulianza mwaka 2105 lakini wakati tukiwa tunaendelea na ujenzi wa upande wa gati kuna changamoto za mgogoro wa  ardhi uliibuka na baada ya kuumaliza, tukaendelea na ujenzi mwaka 2018 na sasa umekamilika.

“Mradi huu kwa ujumla wake umehusisha ujenzi wa gati, jengo la abiria, jengo la kuhifadhia mizigo pamoja na eneo la vyoo na sehemu ya ulinzi. Jumla mradi hu umegharimu Shilingi bilioni 1.265 kama. Matarajio ya mradi huu utaweza kutoa huduma katika visiwa zaidi ya sita ambavyo vinazunguka eneo hili la Lushamba,” alisema

 BANDARI YA MAGARINI

Akizungumza ujenzi wa Bandari ndogo ya Magarini Wilayani Muleba jana, Machindiuza, alisema ulianza mwaka 2018 na kukamilika Agosti 2019 ambapo wananchi wa eneo hilo walioanza kutumia kuanzia Desemba 3, mwaka huu.

Alisema tangu ulipokamilika ujenzi wake wameanza kukusanya mapato ya Serikali huku vyombo vilivyokuwa vikitumia bandari bubu vikihamia katika bandari hiyo kwa ajili ya usalama.

“Bandari hii inahudumia visiwa vya Ikuza na Misenyi ambavyo vipi katika maeneo haya na wananchi wamekuwa wakihitaji masuala mbalimbali ikiwamo wanaishi maeneo hayo wanaendelea kufanya shughuli zao

“Hii ni sehemu zaidi inapitisha mazao kutoka ziwani ambayo ni samaki, dagaa, lakini pia wanabeba mzigo kidogomidogo pamoja na mazao ya vyakula na vifaa vya ujenzi.  Ujenzi mzima wa mradi huu ukitumiwa takribani Sh bilioni 1.73  ambapo tuliweza kujenga gari, jengo la abiri na mzigo pamoja na tanki za maji, vyoo na geti,” alisema

Mkazi wa Kisiwa cha Ikuza, Paul Stephano alisema kuwa kuimarika kwa bandari ya Magarini imekuwa msaada kwao kwa utaratibu wa sasa kila abiri anayepanda kwenye boti hutambuliwa na mamlaka husika.

“Ikuza ni kisiwa kikuwa sana na kina watu wengi ambao hutumia zaidi usafiri wa boti, kwa sasa tupo kwenye hali nzuri sana kwetu tunaishukuru  Serikali kwa kujengea bandari ya kisasa ambayo ni mkombozi kwetu,” alisema Stephano

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles