29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

BANDARI DAR YAANZA KUPANULIWA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA) imeanza kutekeleza mradi wa kuboresha  Bandari ya Dar es Salaam (Dar es Salaam Maritime Gateway Project).

Hatua hiyo inakwenda sambamba na upanuzi wa kina cha Bandari ya Dar es Salaama   kuruhusu meli kubwa za mizigo kutia nanga.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) jana, ilieleza kuwa kwa sasa kazi ya kupima uimara  wa udongo  inaendelea kabla ya kujenga nguzo kwa ajili ya ujenzi wa gati la kuhudumia magari (Ro-Ro berth).

Gati hilo litakuwa na uwezo wa kuhudumia meli zenye urefu wa zaidi ya mita 250 na kina cha mita 14.5 ifikapo mwaka 2022.

Julai 2, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli, aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa mradi wa DMGP   kuimarisha na kuongeza kina cha gaati namba 1-7 kufikia mita 15.

“Mradi huu utakapokamilika utaongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam wa kuhudumia shehena kutoka tani milioni 15 za sasa hadi kufikia tani milioni 28 kwa mwaka.

“Bandari pia itaweza kuhudumia meli kubwa za kisasa zenye uwezo wa kubeba makasha 8,000 kutoka 2,500 ya sasa ifikapo mwaka 2028,” ilieleza taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles