23 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

Bandari Dar kufurika mizigo Novemba

bandariNa MWANDISHI WETU- DAR ES SALAAM

RAIS wa wafanyabiashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) nchini Tanzania, Sumaili Edward, ametangaza kuwa wafanyabiashara wa nchi hiyo wataanza tena kupitisha mizigo yao katika bandari ya Dar es Salaam Oktoba 30, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Edward alisema awali bandari hiyo ilikuwa na changamoto nyingi zilizosababisha washindwe kuitumia.

Alisema wanapojipanga kuanza kutumia bandari ya Dar es Salaam, wanaishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwaondolea vikwazo walivyokuwa wakikabiliana navyo.

“Tumekaa zaidi ya miaka miwili bila kutumia bandari hii kutokana na vikwazo vilivyokuwa nje ya uwezo wetu, moja tatizo la mizani, stoo ya kuhifadhia bidhaa pia tulikuwa hatupati faida kwani kazi ya siku moja ilikuwa  inachukua wiki nzima.

“Tunaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kusikia kilio chetu. Awali  katika bandari hii tulikuwa tunapewa siku 14 za kuhifadhi mizigo lakini hivi sasa siku 30 kwani kuanzia Novemba  mwaka huu bandari itasheheni mizigo mingi sana,” alisema Edward.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles