27.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

BALOZI WA UINGEREZA AZINDUA SOLA

NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM


BALOZI wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Crooke, ameshiriki uzinduzi wa Kampuni ya umeme usiotegemea gridi iitwayo Trend Solar, uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Slipwy.

Uzinduzi huo wa Trend Solar uliambatana na kuingia ubia na Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes ili kutoa umeme na vipindi vya runinga kwa wakazi wa vijijini ambako hawajafikiwa na umeme.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Sarah alisema

Trend itawasaidia watu waliopo vijijini ambako hawajafikiwa na umeme wa gridi kupata umeme na kujinufaisha kielemu na hata kuburudika kwa kuangalia vipindi mbalimbali vya runinga.

“Hii ni fursa ya watoto kujiendeleza kielemu kwa kusoma usiku, lakini pia wataangalia runinga na michezo mbalimbali kama Kombe la Dunia,” alisema Sarah.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Trend Solar, Irfan Mirza, alisema kupitia kampuni hiyo, watawaondolea watu kusahaulika katika maendeleo na wale ambao hawakuwa na fursa ya kuangalia runinga kwa kukosa umeme sasa kufurahia.

“Kupitia Trend Solar tutawaondolea watu tatizo la kusahaulika kwenye maendeleo ya kidigitali, ambapo itawasaidia wale waliokuwa wanakosa fursa ya kusoma na kuangalia vitu mbalimbali kwenye mitandao, sasa kunufaika pamoja na kutazama soka na michezo mingine kwenye runinga,” alisema Irfan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,327FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles