Na Mwandishi Wetu
BALOZI wa Tanzania nchini Algeria, Imani Njalikai amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu wa Afrika (CAAID), Dk. Amine Boutalbi katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano na CAAID ambayo ni kiungo muhimu kati ya ubalozi na sekta binafsi nchini Algeria katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.
Balozi Njalikai amesema ubalozi huo utashirikiana na mamlaka za Tanzania hasa TPSF, TIC na Tantrade ili kufanikisha ushiriki wa wafanyabiashara kwenye makongamano ya uwekezaji na biashara yanayoandaliwa na CAAID, Mei 2024.
Balozi Njalikai ameongeza kuwa watashirikiana na kituo hicho kuratibu kongamano maalumu la wafanyabishara wa Algeria nchini Tanzania mwaka 2024 kwa lengo kuimarisha uwekezaji na biashara kati ya wafanyabiashara wan chi hizo mbili.
Naye Dk. Boutalbi amemhakikishia Balozi Njalikai kuwa CAAID itaratibu ushiriki wa wafanyabiashara wa Algeria kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Saba Saba kwa mwaka 2024.