25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi wa China azungumzia Watanzania wanaosoma nchini humo na corona

Mwandishi wetu -Dar es Salaam

WAKATI watu waliofariki dunia kwa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona nchini China ikifika 259 na mataifa mbalimbali yakiendelea kuthibitisha uwepo wa virusi hivyo kwenye maeneo yao, ubalozi wa China nchini umekutana na Serikali kuzungumzia hali ya raia wa Tanzania haswa wanafunzi walio nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa wizara hiyo Profesa Palamangamba Kabudi, alisema ubalozi wa China umeomba fursa ya kukutana na Serikali kwa nia ya kueleza hali ilivyo nchini China, hatua zinazochukuliwa na Serikali ya China kukabiliana na maradhi hayo ili kuzuia kusambaa katika maeneo mengine duniani na hali ilivyo kwa Watanzania wanaoishi nchini humo.

Kwa upande wa  Balozi wa China nchini, Wu Ke aliwaondoa wasiwasi Watanzania wote wakiwemo Wazazi na Ndugu wa wanafunzi zaidi ya 4,000 wanaosoma China na hususani wanafunzi 400 walioko Hubei  katika Mji wa Wuhan ambapo panatajwa kama kitovu cha virusi vya Corona kwa kusema wako salama na hakuna hata mmoja aliyeathiriwa.

Alisema Serikali ya China kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) linachukua hatua zote kuhakikisha virusi hivyo havisambai katika maeneo mengine hasa baada ya shirika hilo kuutangaza ugonjwa huo kama janga, ikiwemo jitihada za China kujenga Hospitali maalum kwa ajili ya kuwatibu wote watakaoathirika.

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema hadi sasa hakuna rai wa Tanzania ama mgeni aliyeingia nchini ambaye aliyethibitika kuwa na virusi hivyo.

Alisema Serikali inaendelea kuchukua hatua stahiki na za dharura ikiwemo kuwapima watu wote wanaowasili nchini kupitia viwanja vya ndege na aina nyingine za usafiri.

Alisema  tayari serikali kwa kushirikiana na wadau wengine  imeimarisha uwezo wa kuwapima ndani ya nchi mtu yeyote atakayeshukiwa wa virusi hivyo badala ya kupeleka sampuli hizo sehemu nyingine ikiwa ni pamoja na nje ya nchi.

Alisema mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote ama mtu yeyote aliyeshukiwa ama kuthibitishwa kuwa na Virusi vya Corona na tayari Wizara imetenga maeneo manne kwa kuangalia maeneo yaliyoko katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, Mwanza na Kilimanjaro.

Ummy alisema mazungumzo yanaendelea ili Zanzibar nayo iweze kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wagonjwa ama washukiwa wa homa ya Corona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles