24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Balozi Seif awaonya CCM kuachana na makundi

SAM BAHARI-SHINYANGA

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini, wameaswa kuondokana na siasa za makundi baada ya wagombea wao kushindwa katika chaguzi za kura za maoni zinazofanyika ndani ya chama hicho.

Rai hiyo ilitolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, katika maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 42 tangu chama hicho kuasisiwa mwaka 1977.

Balozi Idd ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, alisema changamoto kubwa ambayo hukigharimu chama ni kugeuka kwa wanachama wake baada ya wagombea waliokuwa wanawatarajia kushinda katika kura za maoni lakini wakashindwa na kuanzisha makundi katika chama hicho.   

Alisema licha ya kuanzisha tabia ya siasa za makundi ndani ya chama hicho, lakini mbaya zaidi ni kule wanachama hao kuamua kuwachagua wagombea wa vyama vya upinzani wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Serikali unaohusisha vyama vyote nchini.  

Alisema kutokana na jazba za wanachama hao, huwaibia siri mbalimbali za chama hicho na kusababisha wagombea wa CCM kushindwa katika nafasi mbalimbali wanazoziomba katika uchaguzi mkuu.

“Niwaombe wanachama wenzangu muondokane na siasa za makundi, hebu tuachane na mpango huo na kwamba mgombea wako akishindwa usihame wala kubadili chama unachotakiwa ni kuungana na mgombea wa CCM,” alisema Balozi Idd.

Katika Maadhimisho hayo jumla ya wanachama 40 kutoka vyama mbalimbali vya upinzani walikabidhi kadi zao kwa uongozi wa CCM na wanachama wapya 347 walijiunga na chama hicho. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles