23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

BALOZI LUSINDE ASIMULIA KINGUNGE ALIVYOMGOMEA NYERERE NA KUMVUA CHEO


RAMADHAN HASSAN Na Hastin Liumba - DODOMA/KAHAMA

VIONGOZI na wanasiasa mbalimbali wameendelea kumlilia mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru aliyefariki dunia juzi asubuhi.

Miongoni mwa viongozi hao ni Balozi Job Lusinde ambaye amemzungumzia Kingunge kama alikuwa kiongozi mwenye misimamo na asiyependa kuyumbishwa.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi nyumbani kwake, Balozi Lusinde ambaye amewahi kuwa waziri katika Serikali ya Mwalimu Julius Nyerere akitumikia wizara mbalimbali zikiwamo Serikali za Mitaa na Mambo ya Ndani, alisema amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa, hasa ikizingatiwa kuwa mwanasiasa huyo amelitumikia taifa kwa muda mrefu.

Balozi Lusinde ambaye ndiye waziri pekee wa baraza la kwanza la enzi za Mwalimu Nyerere aliyebaki hai mara baada ya George Kahama kufariki mwaka jana, amekumbusha jinsi ambavyo Kingunge alikuwa na misimamo mikali na mtu pekee ambaye hakuogopa kupingana na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kama kiongozi wake.

“Mfano ambao sitausahau, palikuwa na mjadala katika Bunge wakati huo yeye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida nadhani na alikuwa anaingia katika Bunge.

“Katika mjadala ule tulikuwa tunapiga kura za ndio na hapana, ilipofika kwake alikataa, wakati ule haikuwa sawa kimaadili na kibunge, siku hiyo hiyo Mwalimu  Nyerere alimwondoa katika wadhifa wake, kwahiyo alisimamia misimamo yake,” alisema.

Balozi Lusinde alisema Kingunge alikuwa ni mtu jeuri mwenye msimamo na aliamini anasimamia anachokiamini.

“Hakujali na aliendelea na kazi, baadae akarudi tena serikalini,” alisema.

Balozi Lusinde ambaye amewahi kuwa balozi katika nchi kadhaa ikiwemo China, akielezea jinsi alivyomfahamu Kingunge alisema: “Namfahamu tangu zamani alipokuwa kijana, alipokwenda kusoma Liberia.

“Alikuwa ni kijana mmoja mkakamavu na mwenye nguvu nyingi, alipotoka huko mara moja aliingia katika shughuli za chama toka mwanzo mpaka tumeendelea kuwa nae.”

Alisema pamoja na kwamba alikuwa ametoka ndani ya CCM, lakini yeye binafsi bado alikuwa anaamini ni mwanachama wa CCM.

Balozi Lusinde ambaye ndiye aliyetia saini hati ya Muungano mwaka 1964 akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alisema alizungumza na Kingunge kabla ya kutoka CCM na alimweleza kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ……

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles