26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

BALOZI IDDI: ZALISHENI VIUNGO VYENYE UBORA

 

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi, amewataka Watanzania kuzalisha na kuwekeza zaidi viungo vizuri na vyenye ubora ili kuchangamkia fursa ya masoko nje ya nchi.

Akizungumza katika siku ya viungo iliyofanyika jana katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba, Balozi Iddi alisema kuna viungo vingi vinahitajika katika nchi za Mashariki ya Kati, Asia na baadhi ya nchi za Ulaya, hivyo ni vema wajasiriamali wakazalisha viungo hivyo kwa wingi na kutafuta masoko hayo.

Alisema viungo ni mazao muhimu katika mwili wa binadamu na vimekuwa vikipendwa na idadi kubwa ya watu, hivyo aliwashauri wafanyabiashara watumie fursa hiyo kuhakikisha wanazalisha kwa wingi na kutafuta masoko ya kutosha.

Balozi Iddi aliwataka kuzalisha viungo zaidi kama pilipili mtama, iliki, vanila, mdalasini na vingine, kwani kuna nchi ambazo wana viwanda vya kuchakata viungo lakini wao hawazalishi.

“Watengenezaji wa viungo mjitahidi kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu ili kuondokana na soko la viungo kwenda nje kupitia madalali ambao wanajipatia pesa nyingi inayotokana na kuwanyonya wazalishaj,” alisema Balozi Iddi.

Pia aliwaomba Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kuendelea kuwatafutia masoko watayarishaji wa viungo ili waweze kuuza bidhaa zao na kuongeza uzalishaji.

Naye Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Amina Salum Ally, aliwahakikishia watayarishaji hao wa viungo kuwa Tanzania itahakikisha inarudi katika soko la viungo ambapo hapo awali ilikuwa ya kwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles