Balozi awapa mzuka Simba kuimaliza Platinums

0
641

Na Winfrida Mtoi

Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Profesa Emmanuel Mbennah, amekiongezea mzuka kikosi cha Simba baada ya kuwataka wachezaji waondoe hofu na kufanya kama walichowafanyia Plateau United ya Nigeria.

Balozi ametoa kauli hiyo leo alipokutana na wachezaji wa Simba, walipowasili Zimbabwe kujiandaa na mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinums ya nchini huko utakaochezwa Jumatano ya wiki ijayo.

Balozi Mbennah, amewapongeza wachezaji wa Simba na kusema timu ya waliyokutana nayo awali ya Plateau United haikuwa ya kinyonge, lakini waliweza kuiwakilisha Tanzania.

“Mnacheza vizuri sisi tunawatazama katika runinga mliifunga ile timu ya Nigeria, tunafikiri mtaendelea vizuri kwa sababu hatuna wasiwasi, nadhani kuna Watanzania wengi hapa na sisi tutakuwepo pamoja nanyi,” amesema Balozi Mbennah.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here