22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

BALOZI AIPIGIA CHAPUO BANDARI DAR

Na MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM

BALOZI wa Uganda  nchini, Richard Kabonero amewataka wafanyabiashara wa Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema hiyo ni kwa vile  bandari hiyo kuimarisha ufanisi wake na kutatua changamoto nyingi zilizokuwa zinawakabili wafanyabiashara hao.

Alisema Tanzania na Uganda zimeazimia kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa reli na maji kupitia Ziwa Victoria   kuhakikisha wanatumia gharama nafuu katika biashara ya nchi hizo mbili.

Balozi alisema katika kutimiza lengo hilo, Serikali ya Uganda inajenga bandari kubwa ya Bukasa jijini Kampala na inaimarisha miundombinu yake ya usafirishaji  kuweza kutumia Shorobo ya Kati (Central Corridor) kwa ufanisi.

“Ninaipongeza menejimenti ya TPA kwa kazi kubwa, nzuri na yenye ufanisi mnayoifanya.

“Rais wangu Mheshimiwa Museveni, anaipenda sana bandari ya Dar es Salaam, hivyo wafanyabiashara wetu wataendelea kuitumia bandari hii na kuongeza shehena ya Uganda kupitia hapa,” alisema Balozi huyo.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, alisema shehena ya Uganda kupitia bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikiongezeka tangu mwaka 2017 ambako   tani 165,000 zilihudumiwa wakati mwaka huu  mzigo umeongezeka na kufikia tani 270,000.

Alisema ongezeko hilo linachangiwa na juhudi za Serikali  kuboresha miundombinu na jitihada za  masoko zinazofanywa na menejimenti ya TPA.

“Tunakushuru sana Mheshimiwa Balozi kwa kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya TPA, nchi yako na wafanyabiashara wa Uganda.

“Hivi karibuni pia tumeshuhudia mabalozi wengi wakitutembelea na kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano   kukuza uhusiano katika   uchumi,” alisema Kakoko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles