23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Balotelli adai kutomtambua Klopp

Mario  Balotelli
Mario Balotelli

NICE, UFARANSA

MSHAMBULIAJI wa timu ya Nice, Mario  Balotelli, amedai kutomtambua kocha wa timu yake ya zamani ya  Liverpool, Jurgen Klopp, ambaye alimtimua katika timu hiyo.

Balotelli alisajiliwa na kocha wa zamani wa timu hiyo, Brendan Rodgers, mwaka  2015 akitokea timu ya  AC Milan lakini alishindwa kuwa na ushawishi kwa kocha huyo na kurejea Milan kwa mkopo wa muda mfupi.

Nyota huyo anayecheza timu ya Nice amefunga mabao sita katika michezo mitano ya kwanza ya Ligi Kuu Ufaransa ya msimu huu, baada ya kusajiliwa  dirisha lililopita akiwa mchezaji huru.

Balotelli alisema hakuna nafasi ya kurejea katika timu ya Liverpool baada ya Klopp kudai wapo tayari kumpokea nyota huyo baada ya kurejea katika kiwango chake.

“Klopp? Simjui, aliniambia niondoke Liverpool kwa mkopo na kurejea lakini nikamwambia hakuna kitu kama hicho.

“Wakati nikiwa katika klabu hiyo sikuwa na uhusiano mzuri na Klopp na hata alivyonitimua na kuniambia nitarejea sikuwa tayari na jambo hilo,” alisema Balotelli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles