27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Bakwata yatoa siri ya Uchaguzi Mkuu

SheikhHasanChizengaaNA BENJAMIN MASESE, MWANZA

 

BARAZA la Waislamu Tanzania (BAKWATA), limefanya uchunguzi na kugundua kuwa Waislamu watamchagua rais asiye na uchungu na nchi yake kwa sababu hawahudhurii mikutano ya kampeni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Haamid Jongo, alisema kutokana na uchunguzi huo, amewataka Waislamu wote nchini kuhudhuria mikutano ya wagombea wote wa nafasi ya urais bila kujali ukubwa wake ili kusikiliza sera  badala ya kusubiria kusoma mitandaoni na kusikiliza kupitia vyombo vya habari.

 

Jongo ambaye hakubainisha jinsi walivyofanya uchunguzi wao, alisema wamebaini baadhi ya wagombea nafasi ya urais wanataka nafasi hiyo kwa ajili ya heshima na si kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo.

Alisema lengo la kuwataka kwenda kusikiliza sera za wagombea urais wa vyama vyote ni kumpata kiongozi mpenda maendeleo na mwenye moyo unaofanana  na aliyewahi kuwa Rais wa Afrika Kusini, marehemu Nelson Mandela na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

 

“Tanzania ni nchi ya amani na utulivu, hivyo tunataka kiongozi anayeweza kufanya uamuzi mgumu, sasa tutampata kiongozi huyo kwa kwenda kusikiliza sera za wagombea majukwaani na si vijiweni, tunahitaji mabadiliko ya maendeleo na siyo kwenda Ikulu kutafuta heshima ya kupigiwa mizinga.

“Leo nawalenga Waislamu tu kwa kuwapa wito kwamba wasishangilie nyimbo za  wasanii wanaotembea na wagombea, wasikilize wagombea wenyewe, kama Bakwata hatuungi kauli za kudai kwamba hakuna kilichofanyika kwa miaka 54 ya uhuru, yapo yamefanyika kwa kiwango fulani.

 

“Hizi changamoto zinazotukabili Watanzania ni za kawaida, maana maendeleo huzaa changamoto, zipo nchi zimeendelea kiuchumi lakini watu wake wanajinyonga kutokana na kubaliwa na changamoto, Tanzania haipo peponi kiasi cha kuwaambia Watanzania kwamba akiingia madarakani hakuna tena umasikini, hakuna mtu anayeweza kumaliza umasikini wa mtu bali ni kupunguza tu,” alisema Jongo.

Alisema wapo baadhi ya wagombea wa nafasi ya urais wanaonyesha wanataka nafasi hiyo ili kutafuta heshima, kitendo kinachowapa wasiwasi Watanzania kutopata kiongozi atakayepunguza changamoto zinazowakabili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles