32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Bakwata yataka Watanzania wajiandae kunufaika

selemani-lolilaNA HADIA KHAMIS- DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata),  Selemani Lolila, amesema Tanzania ijiandae kunufaika kibiashara na kukuza uchumi wa taifa.

Kutokana na hali hiyo, alisema kila Mtanzania atanufaika na bidhaa zenye nembo ya Halal ambapo wapo mbioni kuingia kwenye orodha ya nchi 33 ambazo zinatumia bidhaa halal za vyakula.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Lolila alisema nembo ya Halal itaweza kumhakikishia mlaji Muislamu  na wasiokuwa Waislamu uhakika wa chakula tangu kilipotoka hadi kilipofikia.

“Katika kitabu cha Qur’an kinatueleza kuwa tuchinje na tule vyakula halal, lakini kwa sababu mbalimbali tumekuwa tukila chakula bila kujua kimeanzia wapi na kimepita katika njia gani.

“Kwa kutambua mchango wa dini yetu, tumepata mafunzo kutoka kwa viongozi wa JAKIM ya nchini Malaysia ambao ndio wamiliki wa nembo ya Halal, baada ya mwaka mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa kile walichotuachia ili kupata nembo hiyo itakayotusaidia kuuza bidhaa zetu katika nchi za Asia na nyinginezo, “alisema Lolila.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halal Tanzania, Muhsin Hussein, alisema mafunzo waliyopatiwa ni ya bidhaa zinazozalishwa nchini ambazo zitatoa fursa ya kuuzwa nje ya nchi.

Alisema kwa sasa wanatarajia kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili waweze kuuhabarisha umma katika suala zima la kutumia bidhaa zilizowekwa nembo ya Halal.

“Kama tutafanikiwa kupata nembo ya Halal, hatuna maana ya kuwa nembo za Serikali zilizowekwa kisheria kwamba hazitakuwepo katika bidhaa zetu, bali nembo zote zitakuwepo kama sheria ya vyakula inavyoeleza, kwa kutambua hilo katika mafunzo haya tumeungana na wawakilishi wa TBS pamoja na TFDA ili kujionea tunachojifunza,” alisema Lolila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles