30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Bakwata yaagiza swala ya Idd kuswaliwa Manyema

 CHRISTINA GAULUHANGA -DAR ES SALAAM 

BARAZA la Ulamaa Taifa, limewataka viongozi wa Baraza la Kiislam Tanzania Taifa (Bakwata), viongozi wa Kiserikali na waumini wa Msikitini wa Manyema kuswali Idd kwenye msikitini huo uliopo Kariakoo jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Baraza la Ulamaa Taifa, Sheikh Hassan Chizenga alisema kuwa kwa mwaka huu hakutakuwa na swala ya Kitaifa ya Idd Wala Baraza la Idd Ila kila msikiti utaswali Idd ili kuepuka msongomano. 

Alisema katika Msikiti wa Manyema ambapo pataswaliwa na viongozi kutatolewa salamu za Idd na nasaha za kitaifa. 

“Tumemzoea kuswali swala ya Idd kwa kujumuika pamoja misikiti kadhaa lakini kwa sababu ya ugonjwa huu wa corona, tumelazimika kuweka mikakati hii,” alisema Sheikh Chizenga. 

Pamoja na hali hiyo alisisitiza hakutakuwa na Baraza la Idd mikoani, wilayani au kwenye kata hivyo ni marufuku kwa msikiti wowote au kundi lolote kuandaa baraza la Idd El Fitri.

Chizenga alisema kuhusu mkesha wa usiku wa cheo misikiti yote yenye utaratibu wa kuendeshwa inaruhusiwa kuendelea isipokuwa kwa sharti la kuzingatia utaratibu wa afya. 

Pia alisema kila muumini katika mkesha huo anatakiwa kwenda na daku yake kwani hakutakuwa na chakula cha pamoja kama ilivyozoeleka ili kuondoa misongamano inayoweza kuchangia maambukizi. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles