27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

BAKAMBU MCHEZAJI GHALI AFRIKA

BEIJING, CHINA


MSHAMBULIAJI wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Cedric Bakambu, amekamilisha kuhamia klabu ya Beijing Guoan ya China na kuwa mchezaji ghali zaidi kutoka Afrika kwa sasa.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya soka nchini China, haijatangaza hadharani kiasi cha fedha alizonunuliwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, lakini imesema ni zaidi ya dola milioni 90 za Marekani.

Kiwango hicho kinashinda kile cha dola milioni 77 ambazo zilitolewa kumnunua mchezaji wa Arsenal, Pierre- Emerick Aubameyang wa Gabon.

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Sport, Bakambu, amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia timu hiyo.

Timu ya Beijing Guoan, ambayo ilimaliza nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu ya China yenye timu 16, ilikuwa imetarajia kulipa kiasi kidogo cha fedha kwa mchezaji huyo aliyeondoka Villarreal ya Hispania Januari mwaka huu, baada ya kulipa dola milioni 50 ili kuvunja mkataba wake.

Bakambu ndiye mchezaji pekee wa soka Afrika kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi katika Ligi Kuu ya Hispania, alikuwa miongoni mwa wafungaji mabao bora La Liga na alifunga mabao 9  hadi anaondoka Villarreal.

Alijiunga na klabu hiyo mwaka 2015 akitokea timu ya Uturuki, Bursaspor, ambapo alifunga jumla ya mabao 21 msimu mmoja aliokuwa katika timu hiyo.

Bakambu ni mzaliwa wa Ufaransa na alichezea timu ya taifa ya Ufaransa ya vijana kabla ya kubadilisha uamuzi na kuamua kuichezea DRC mwaka 2015.

Mchezaji huyo hadi sasa amefungia timu ya taifa ya DRC mabao saba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,409FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles