28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Babu wa miaka 94 ajinyonga

YOHANA PAUL Na FATUMA SAID – MWANZA

BABU wa miaka 94 ameripotiwa kujinyonga hadi kufariki dunia jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema marehemu hajatambuliwa jina lake.

Muliro alisema kuwa marehemu alikutwa amejinyonga kwa kutumia mtandio uliofungwa juu ya mti wa mwembe pembezoni mwa nyumba yake.

Alisema chanzo cha kifo chake hakijulikani na polisi wanaendelea na uchunguzi.

Katika hatua nyingine, Muliro alisema kuwa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watuhumiwa 12 kwa kuhusishwa na matukio ya mauaji na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Kati ya watuhumiwa hao, wanne wanatuhumiwa kubaka na kumsababishia kifo mwanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mahina.

Kamanda Muliro alisema watuhumiwa wanne wanashikiliwa kwa tuhuma za kubaka na kusababishia kifo cha mwanafunzi huyo aliyefariki dunia Agosti 15, mwaka huu eneo la Mahina na mwili wake kukutwa juu ya mawe.

Aliwataja watuhumiwa hao ni Sospeter Kazumari (37), Justine John (24), Amosi Andrea (36) na Rebeka Bukindu (35).

Alisema mtuhumiwa mwingine, Joseph Msafiri (30) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Namabungo wilayani Ukerewe, anahusishwa na mauaji ya mwanafunzi wa kidato cha tatu, Euzebia Didukus (16) wa Shule ya Sekondari Nansio aliyekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Katika tukio jingine, jeshi hilo limewakamata watuhumiwa saba kwa kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, wawili kati yao walikutwa na gramu 10 za heroine na watano wakikamatwa na kilo 30 za bangi.

Waliokamatwa ni Elizabeth Lucas na Hamza Haruna wakazi wa Mtaa wa Mwinuko  na Herena Nagambona, Yahaya Haruna, Shabaan Said, Nestory Moses na Zainabu Zakaria wote wakazi wa Mtaa wa Mwananchi wilayani Ilemela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles