22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Baba wa Makamu Mwenyekiti CUF ajiunga na ACT

Mwandishi Wetu, Zanzibar

Baba mzazi wa Makamu Mwenyekiti mpya wa Chama cha Wananchi (CUF), Abassi Juma Muhunzi, mzee Juma Muhunzi, amechukua kadi ya ACT-Wazalendo huku akibubujikwa machozi jambo lililosababisha mamia ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo kuibuka kwa shangwe.

Tukio hilo limetokea leo Jumamosi Machi23, katika eneo la Ngezi Chambani katika Wilaya ya mkoani iliyopo Kusini Pemba ambapo Maalim Seif Sharif Hamad alifika ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuhama CUF.

Zoezi la kugawa kadi lililokuwa likiendeshwa na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe, lilipoanza wa kwanza kupewa kadi alikuwa mzee Muhunzi ambaye alikuwa ameambatana na baadhi ya wanafamilia.

Mzee huyo alinyanyuka kwenye kiti chake huku akitokwa na machozi alipopokea kadi hiyo na kisha kurudi kuketi huku baadhi ya wanafamilia wakifuatia kupokea kadi.

Viongozi wote wa CUF wilaya hiyo wamejiunga na ACT-Wazalendo, huku wanachama wengine wakielezwa watapewa utaratibu wa kupata kadi kwenye matawi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles