21.1 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Baba wa kambo amcharanga mapanga mtoto wa miaka mitatu

NYEMO MALECELA -KAGERA

JESHI la Polisi Mkoani Kagera linamshikiria Leonard Kishenya (36) kwa tuhuma za kumuua mtoto wa mke wake wa miaka mitatu kwa kumcharanga mapanga na kumtenganisha viungo vyake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema tukio hilo lilitokea usiku wa mkesha wa mwaka mpya saa 6.40 usiku katika Kijiji cha Katorerwa Tarafa ya Kiziba wilayani Misenyi Mkoani Kagera.

Kwa mujibu wa Kamanda Malimi, Leonard alimcharanga mapanga Careen Crispine (3) baada ya kutokea ugomvi kati yake na  mkewe huyo Domina Andrew (30).

Malimi alisema mauaji hayo yalitokea baada ya wanandoa hao kutoka katika matembezi ya mkesha wa mwaka mpya ambako walikuwa wameenda kuywa pombe.

Alisema baada ya kurudi nyumbani walianza kugombana na kusababisha mama mzazi wa mtoto huyo kukimbilia kwa jirani kwa lengo la kunusuru maisha yake na kumuacha mwanae nyumbani pamoja na mume wake.

“Wakati Domina anakimbia nyumbani alimuacha mwanae akiwa amelala usingizi na aliporudi nyumbani saa moja asubuhi alimkuta mwanae Careen akiwa ameuliwa kwa kucharangwa mapanga kwa kujeruhiwa kichwani na kukatwa mkono wa kushoto ambao ulikuwa umetenganishwa na mwili na mwanaume akiwa tayari ametoweka nyumbani,” alisema.

Malimi alisema Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo jana (juzi) akiwa amejificha na uchunguzi wa mauaji hayo unaendelea, ukikamilika atafikishwa mahakamani kwa ajili ya kuchukuliwa na hatua ya kisheria.

“Hadi sasa haijulikani chanzo cha mtuhumiwa kumuua mtoto huyo ambaye ni malaika japokuwa kwa mtazamo wa kawaida wivu wa mapenzi ndio chanzo cha ugomvi huo,” alisema.

Katika taarifa aliyoitoa mwishoni mwa mwaka jana, Malimi alisema makosa ya mauaji na ubakaji yaliongezeka ukilinganisha na mwaka juzi.

Alisema chanzo kikuu cha makosa ya mengi ya mauaji ni migogoro ya mashamba, mali za urithi, wivu wa mapenzi, kulipa kisasi, ugomvi unaotokana na ulevi kwa kiasi kidogo imani za kishirikina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles