31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Baba mzazi wa mwanafunzi shujaa aibukia hafla ya kumpongeza mwanawe

Derick Milton, Simiyu

Baba mzazi wa mwanafunzi shujaa Yohana Lameck, aliyepata daraja la kwanza na pointi saba, Lameck Lugedenga ameibuka katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne mwaka jana, mkoani Simiyu.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baba huyo alibadilisha hali ya utulivu katika Ukumbi wa Kusekwa Mjini Bariadi ilikofanyika hafla hiyo leo Alhamisi Januari 30, baada ya kutambulishwa kama baba mzazi wa Yohana na kuzua gumzo na minong’ono kutoka kwa watu waliohudhuria hafla hiyo.

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba baba huyo alidaiwa kumtelekeza Yohana na mama yake Mariamu Lulyalya zaidi ya miaka saba na kukimbilia mkoani Morogoro ambako anadaiwa kuishi hadi sasa na hii ni mara ya kwanza kwa baba huyo kuonekana akiwa pamoja na familia yake tangu wakati huo.

Yohana aliibuka mwanafunzi kinara katika mkoa huo kwenye matokeo hayo ya kidato cha nne kwa kupata daraja la kwanza alama A katika masomo yote tisa, huku akiishi mazingira magumu yeye na mama yake tangu baba yake amtelekeze.

Kwa mujibu wa Yohana, baba yake alimtelekeza toka akiwa darasa la nne Shule ya Msingi Igaganulwa, kutokana na umaskini na ilidaiwa alikimbilia mkoani Morogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles