Baba jela miaka mitano kwa kukeketa watoto wake

0
316

Na KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MKAZI wa Kivule wilayani Ilala, Dar es Salaam, Cosmas Chacha (45), amehukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kuwakeketa watoto wake watatu na kuwasababishia majeraha.

Mshtakiwa alihukumiwa jana na  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Rashid Chaungu baada ya mahakama kujiridhisha kwamba alitenda makosa hayo.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi sita na vielelezo vitatu huku mshtakiwa akijitetea mwenyewe.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Chaungu alisema upande wa Jamhuri umeweza kuthibitisha mashtaka bila kuacha shaka yoyote hivyo mahakama imemtia hatiani kwa makosa matatu.

Alisema kila kosa mshtakiwa atakwenda jela miaka mitano, atalipa fidia ya jumla Sh milioni tatu na adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.

Katika hati ya mashtaka inadaiwa, Desemba 8, mwaka jana maeneo ya Kivule mshtakiwa aliwakeketa watoto wake watatu wenye umri chini ya miaka 18 na kuwasababishia majeraha makubwa.

Mshtakiwa alichukua watoto hao kwa ndugu walipokuwa wanalelewa na kuahidi kuwatunza lakini badala yake aliwakeketa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here