24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Baba asakwa kwa kumbaka binti yake

Na Ahmed Makongo -Bunda

POLISI wilayani Bunda Mkoa wa Mara inamsaka Magige Igone, kwa madai ya kumbaka binti yake ambaye pia ni mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Miembeni B iliyoko Halmashauri ya Mji wa Bunda.

Mkuu wa Kituo cha Polisi Nyamuswa, Simon Joseph, akisimulia tukio hilo juzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, aliyekuwa na wajumbe wa kamati ya maadili ya mahakama katika wilaya hiyo, alidai kuwa Igone alimbaka mtoto wake hivi karibuni nyumbani kwake katika Kijiji cha Nyamuswa majira ya usiku.

Kwa upande wake, mtoto huyo akisimulia tukio hilo alidai kuwa baba yake alianza kumtongoza akisema atampatia Sh 5,000 na alipomkatalia ndipo usiku alipomvamia ndani ya chumba chake na kumkamata kwa nguvu huku akiwa amemziba mdomo kwa mikono yake.

Alidai kuwa siku hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa baba yake kumfanyia ukatili huo na kwamba baada ya kufanyiwa kitendo hicho alikimbia na kupiga yowe, na shangazi yake alifika kumchukua na akamlazimisha kuoga ili asionekane kama amebakwa.

“Hii ni mara ya pili baba ananibaka, siku ya kwanza alinifanyia hivyo akaniambia kama nikisema sehemu yoyote ataniua. Sasa ile siku ya pili aliniambia anipe Sh 5,000 tulale naye, nikakataa ndipo usiku akanigongea mlango eti akiomba maji ya kunywa.

“Mimi nikamwambia ‘baba si maji unayo huko’ akanilazimisha ndipo nikafungua na kumpatia maji, nilivyotaka kufunga mlango akaweka mkono wake nikashindwa kuufunga, ndipo aliponivamia kwa nguvu na kunifanya kitendo hicho,” alidai mwanafunzi huyo.

Kwa upande wao polisi walisema shangazi ya binti huyo alikamatwa na kwamba wanaendelea kumsaka baba yake ambaye alitoroka.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bupilipili, alilitaka Jeshi la Polisi wilayani hapa kumsaka mwanaume huyo ili afikishwe kwenye vyombo sharia kujibu tuhuma zinazomkabili.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles