23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Baba amtaka Mayweather kupigana na Amir Khan

Floyd Mayweather Jr., Robert GuerreroLAS VEGAS, MAREKANI
BAADA ya bondia Floyd Mayweather kuchukua ubingwa wa pambano la masumbwi dhidi ya Manny Pacquiao Mei 3 mwaka huu, baba wa bondia huyo amemtaka mwanawe kupigana na Amir Khan katika pambano lake la mwisho.
Mayweather amesisitiza kuwa Septemba mwaka huu anatarajia kustaafu ngumi, hivyo anahitaji pambano moja la mwisho ili kuweza kuachana na mchezo huo, ambapo baba yake anaona bora mwanawe apigane na Amir Khan.
Baba wa Mayweather anaamini kuwa Amir Khan hana uwezo mkubwa wa kuweza kumpiga mwanawe ambaye amefanikiwa kuchukua mkanda wa WBC Welterweight dhidi ya Pacquiao.
“Ninachokifikiria mwanangu apate pambano jepesi Septemba ili aweze kustaafu vizuri, kwa sasa hahitaji pambano gumu sana kwa kuwa tayari amepigana mapambano mengi magumu, lakini kwa sasa kwa kuwa anataka kustaafu ni bora atafute pambano rahisi.
“Ninaamini pambano sahihi litakuwa dhidi ya Amir Khan, mwanangu ana uwezo mkubwa wa kuweza kupambana na Khan na kushinda kwa urahisi tofauti na pambano la Pacquiao,” alisema baba wa Mayweather.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles