29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Baadhi ya majimbo yafutiwa uchaguzi nchini India

Maafisa wa uchaguzi nchini India wamefuta uchaguzi katika eneo la Kusini la nchi hiyo baada ya kukamata fedha zaidi ya dolla milioni 1.5 wanazoamini zilikusudiwa kutumika katika kushawishi mwelekeo wa matokeo.

Maafisa wanasema ni mara ya kwanza uchaguzi kufutwa katika mchakato wa kitaifa wa uchaguzi kufuatia tukio la kujaribu kununua kura.

Uamuzi huo umekuja wakati raia wa India wakiendelea kupiga kura katika uchaguzi wa kitaifa unaofanyika kwa awamu kadhaa, ambapo awamu inayofuata itaanza kesho Alhamis.

Uchaguzi uliofutwa ni wa eneo la Vellora katika jimbo la pwani la Tamil Nadu.Fedha zilizokamatwa ziligundulika kwa wagombea wanaoshiriki katika uchaguzi huo.

Kadhalika uchaguzi umeahirishwa kwa siku tano katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Kaskazini Mashariki kufuatia hofu ya kiusalama.

Takriban watu milioni 900 wana haki ya kupiga kura kuchagua wabunge 543 katika matokeo yanayotarajiwa kutangazwa Mei 23.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles