Baada ya kukosa ubingwa  Hamilton  awatupia lawama Mercedes

0
551

Lewis HamiltonKUALA LUMPUR, MALAYSIA

BINGWA wa mbio za magari Lewis Hamilton ‘Langalanga’, juzi usiku alijikuta akipoteza matumaini ya ubingwa wa Malaysia Grand Prix, baada ya mashine ya gari lake la Kampuni ya Mercedes kuharibika na kushindwa kuendelea na mashindano  hayo.

Daniel Ricciardo ndiye aliyekuwa  bingwa wa michuano hiyo, huku Hamilton akishika nafasi ya pili.

Mshiriki mwingine, Nico Rosberg, alimaliza akiwa nafasi  ya tatu na pointi 23, huku akibakiwa na mizungu mitano iliyomfanya apoteze pointi 125. Ricciardo ambaye ni bingwa wa mbio hizo, alimshinda  Max Verstappen wa Kampuni ya Magari ya  Red Bull.

Baada ya mbio hizo,  Hamilton alilalamika kuhusu  Kampuni ya  Mercedes kushindwa kumpa gari lenye mashine ya uhakika ambayo lingeweza kumudu  mikiki ya wapinzani wake.

“Swali langu kwa Mercedes ni, inakuaje tunatengeza  mashine nyingi lakini ya kwangu ni miongoni mwa zilizoshindwa  kuonesha ubora mwaka huu?

“Ni lazima nipate jibu la tatizo hili kwa sababu halikubaliki, tunapambana ili kuwa mabingwa, kwa nini mashine yangu  tu ishindwe na ionekane si sahihi kwa ajili yangu,” alihoji Hamilton.

Hamilton  alikuwa na matarajio makubwa ya kushinda mbio hizo ambazo zilionekana kuwa na ushindani mkali kabla ya kuanza kusumbuliwa na mashine ya gari lake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here