AZZAN: NIMEZUNGUKWA NA MAADUI

0
377

MBUNGE wa zamani wa Kinondoni, Iddy Azzan, amesema kuwa amezungukwa na maadui wengi ambao wanaweza kusema lolote baya juu yake kwani ni muda mrefu tangu ameanza kuzungumziwa kuhusu dawa za kulevya.

“Mimi tangu nianze kuzungumzwa, sijaanza leo, wanasikiliza kwenye mitandao ya kijamii, hawajui nina maadui wangapi ambao wananizunguka, utakuta mtu  ananitaja kwa chuki zake binafsi ambazo kuthibitisha hawezi,” alisema Azzan.

Alisema polisi walifika nyumbani kwake na kupekuwa, lakini hawakukuta kitu chochote, hivyo anasubiri baadae watamwambia kitu gani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here