25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

AZZAN: NI TUHUMA ZA TANGU 2013

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

MBUNGE wa zamani wa Kinondoni, Idd Azzan (CCM), amesema tuhuma kwamba anahusika na biashara ya dawa za kulevya ni za tangu mwaka 2013.

Azzan alisema hayo alipotakiwa na gazeti hili kuzungumzia suala hilo baada ya kutajwa katika orodha ya watu 65 waliotakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kesho kuhusiana na biashara ya dawa za kulevya.

“Sasa mimi sitaki kuzizungumzia kwa sababu sijui kwanza nilichoitiwa, na hizo tuhuma kwangu zilishatoka tangu 2013 na baadhi ya viongozi wa CCM walisema na zilichukuliwa hatua kipindi kile, kwa hiyo siwezi kusema chochote juu ya hilo kwa kweli,” alisema Azzan.

Alipoelezwa kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amelitaja jina lake kwenye orodha ya watu wanaohusishwa na biashara ya dawa za kulevya ambao wanatakiwa kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi, Azzan alijibu: “ Basi aende akaseme vizuri.

“Kama ningekuwa nafanya hiyo biashara, nafikiri ingekuwa ni rahisi kunikamata na kuniweka ndani, lakini tuache kama ilivyo keshokutwa (kesho) ndiyo nitajua na hapo ndiyo nitasema kitu, lakini kwa sasa tuliache tu.”

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,953FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles