24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

AZIMIO LA ARUSHA SI MZAHA – PROF. SHIVJI

Na AGATHA CHARLES,


WATANZANIA wameshauriwa kuenzi na kuendeleza Azimio la Arusha kwa kutathimini tulipo na tuendako ukiacha changamoto mbalimmbali zinazolikabilia.

Hayo yalizungumzwa kwa nyakati tofauti jana wakati wa mihadhara, simulizi na mijadala iliyofanyika wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha iliyofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dar es Salaam.

Katika mjadala huo, Mkurugenzi wa Kavazi la Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji alisema Azimio la Arusha si mzaha na wala si kitabu kitakatifu ambacho hakiwezi kubadilishwa kuendana na wakati.

Profesa Shivji alisema Azimo la Arusha litaendelea kujadiliwa kwa kuwa linajadilika kutokana na kuwepo wapenzi wa azimio hilo.

“Wapo wapenzi, wanaolipinga, wanafiki na wachache wanaojadili azimio ambao hawageuki nyuma, wanaendelea kupanda mlima,” alisema Profesa Shivji.

Katika mjadala huo, Profesa Shivji alisoma barua aliyosema imeandikwa na mtu aliyemtambulisha kama Issa bin Mariam ambayo alimwandikia mpenzi wake, maudhui yakiwa ni kulilia azimio la Arusha.

Katika barua hiyo, mwandishi Issa alisema pamoja na kuaminika kuwa Azimio lilikufa na kuzikwa baharini lakini ipo siku mzimu wake utafufuka kwani sifa zake zilikuwa taswira na tumaini kwa wanyonge.

Pamoja na kuelezea umuhimu wa azimio pamoja na namna lilivyotelekezwa, mwandishi wa barua hiyo aliapa kuendelea kulilinda Azimio hilo.

Masha

Awali akisimulia namna Azimio la Arusha lilivyopitishwa, Dk Fortunatus Masha ambaye mwaka 1967 alikuwa Katibu Mwenezi na Habari wa Chama cha TANU, alisema moja ya vitu vilivyomsukuma Mwalimu Julius Nyerere wakati huo kulitangaza ni kutafuta itikadi baada ya kuwepo nguvu ya kiutawala kwa mataifa makubwa.

 “1967 baada ya majaribio mengi, moja ya mambo yaliyomgusa Mwalimu ni katika mipango iliyokuwepo ya miaka mitatu, mitano, Watanzania walikuwa tayari kufanya lakini kwa Itikadi gani?” alisema Masha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles