23 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Azealia Banks amuomba radhi Zayn Malik

azealia-banksNEW YORK, MAREKANI

RAPA Azealia Banks, amemwomba radhi msanii anayeunda kundi la ‘One Direction’ Zayn Malik, baada ya kumtolea maneno ya kibaguzi kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.

Azealia alitumia akaunti yake ya Twitter miezi saba iliyopita kumshambulia msanii huyo, lakini wiki iliyopita aliamua kuomba radhi mara, baada ya Twitter kumfungia akaunti yake kutokana na ubaguzi huo.

Kupitia akaunti ya Instagram, Azealia amendika: “Mpendwa Zayn, hakuna neno lolote ambalo naweza kukuambia ili unielewe kwamba naomba msamaha. Kwa matukio ya hivi karibuni yamenifundisha umuhimu wa kuwajibika kwa vitendo nilivyovifanya. Ninachokitaka kwako ni kuomba msamaha, nilifanya makosa.

“Nikiwa kama mwanamke mweusi ndani ya Marekani, wakati mwingine ni kusahau kwamba kuna maneno au maoni ya kuumiza jamii nyingine, wakati mwingine nadhani ni kutokana na mapambano yangu mwenyewe katika mbio za mafanikio,” aliandika Azealia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles