26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Azam yaziombea njaa Simba, Yanga

azam fcNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Azam FC, umetamba kurejea kileleni kwa kishindo kwa kuziombea njaa timu za Simba na Yanga zipoteze kwenye michezo iliyobakia ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Azam ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kucheza michezo 19 na kufanikiwa kufikisha pointi 42, Jumamosi hii inatarajia kucheza mchezo wake wa 17 ugenini dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Wakati timu hiyo ikijiandaa kukabiliana na Mbeya City, vinara wa ligi hiyo Simba na Yanga watakuwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kukamilisha mchezo wa 20 kwa Simba na Yanga wa 19 ambao utakuwa muhimu kwa kila timu ili kupata nafasi ya kuongoza.

Akizungumza na MTANZANIA, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Saad Kawemba, alisema mchezo dhidi ya Mbeya City utawafanya kurudi kwenye mstari baada ya kupata kichapo cha bao 1-0 dhidi ya timu ya Coastal Union.

“Adui yako muombee njaa, huo ndio utaratibu wa ligi, unapopoteza mwingine anachukua nafasi,” alisema Kawemba.

Kawemba alisema japokuwa rekodi yao ya kutofungwa michezo 18 imevurugwa na Coastal Union, wamejipanga kuhakikisha wanapambana ili kurejea  nafasi ya juu ya msimamo wa ligi hiyo.

“Tutarudi kwenye rekodi yetu ya ugenini muda si mrefu, wabaya wetu ambao wanasubiri tufungwe ndio wazungumze watasubiri sana,” alisema Kawemba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles