25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Azam yang’ang’aniwa na Prisons Dar

Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

TIMU ya Azam imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana Uwanja wa Uhuru,  Dar es Salaam.

Azam ilikuwa ya kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 44 kupitia kwa Obrey Chirwa, aliyeunganisha kona fupi iliyopigwa na Bruce Kangwa.

Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili, mshambulizi yalikuwa yakupokezana.

Hata hivyo, Prisons ilifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Elifadhili Jumanne aliyefunga kwa kichwa na matokeo baada ya dakika 90 kuwa sare ya bao 1-1.

Michezo mingine ya ligi hiyo iliyochezwa jana,  Ndanda ikiwa nyumbaniUwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara, iliichapa Mbao mabao 3-0.

Kagera Sugar iliutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Kaitaba ulioko mjini Bukoba kuitandika mabao 2-1 Mwadui.

Mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Yusuph Mhilu dakika ya 12 na Kelvin Sabato dakika ya 38.

Bao pekee la Mwadui FC lilifungwa dakika ya 45 na Omary Daga.

Dimba la Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, wenyeji  Namungo walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Alliance, wakati Ruvu Shooting iliitandika Mtibwa Sugar bao 1-0,  Uwanja wa Mabatini Pwani.

KMC iliwika ugenini Uwanja wa Samora mjini Iringa , baada ya kuifunga Mbeya City bao 1-0, huku Biashara United ikiichapa  Singida United mabao 2-1, Uwanja wa Karume Mara.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles