23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

AZAM YAMWAGA MABILIONI Ni tenda kuonyesha ‘live’ Ligi Kuu

Mkataba mpya
Mkataba mpya

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Azam Media imeongeza mkataba wa udhamini wa miaka mitano wa kurusha moja kwa moja matangazo ya mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya Sh bilioni 23.

Awali, kampuni hiyo iliingia mkataba wa miaka mitatu kudhamini matangazo ya kurusha moja kwa moja baadhi ya mechi za ligi hiyo ambayo ilishirikisha jumla ya timu 16 msimu uliopita.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura, alisema klabu za Ligi Kuu zitanufaika kwa kupata asilimia 70 ya udhamini huo ambapo asilimia iliyobaki itatumika kwa gharama ya uendeshaji wa ligi.

Alisema katika udhamini wa msimu wa ligi wa 2016/17 kiasi cha Sh bilioni 4.1 kitatumika na kila klabu itapata mgawo wa Sh milioni 126 katika vipindi vitatu, ambapo timu zitapewa Sh milioni 42 katika robo ya kwanza.

Alisema katika mgawanyo huo, kiasi kitakachotolewa katika robo ya mwisho kabla ya ligi kumalizika kitatofautiana kulingana na msimamo wa ligi utakavyokuwa, kwani timu itakayotwaa ubingwa itapata fedha nyingi kuliko ile inayoshuka daraja.

Wambura aliongeza kuwa gharama zitakazotumika kwenye kila msimu wa ligi kwa miaka mitano ya udhamini zitakuwa zikiongezeka.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando, alisema udhamini huo utaziongezea klabu nguvu na kuzisaidia kukuza ligi na kufanya vizuri.

“Tutahakikisha tunarekebisha mapungufu yaliyojitokeza msimu uliopita na kupambana na changamoto zote na kuwaonyesha Watanzania kwamba Azam ina dhamira ya dhati ya kuweza kufanya kazi kwa ubora zaidi,” alisema.

Msimu uliopita timu 16 zilizoshiriki Ligi Kuu zilipata mgawo wa Sh milioni 100 kila moja kutoka katika udhamini huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles