23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Azam yaipuuza Yanga kwa Tchetche

000NA MWANDISHI WETU

MABINGWA wa Kombe la Kagame, timu ya Azam imeshtushwa na taarifa za uongozi wa Yanga kumfungia kazi mshambuliaji wake tegemeo, Kipre Tchetche, ili kumsajili kwenye dirisha dogo la usajili linalofunguliwa Jumapili hii.

Uongozi wa Azam jana umesema kuwa mshambuliaji huyo bado yupo kwenye mipango ya muda mrefu ya benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu Stewart Hall na ataendelea kuwepo sana ndani ya timu hiyo.

Tchetche amekuwa mwiba mkali kwa timu pinzani, mpaka sasa akiwa ameshafunga jumla ya mabao sita kwenye mechi tisa walizocheza za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu.

Moja ya mabao hayo ni lile alilotupia walipocheza na Yanga Oktoba 17, mwaka huu kwenye sare ya 1-1, akiisawazishia timu yake alipoingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Allan Wanga.

Mtendaji Mkuu wa timu ya Azam FC, Saad Kawemba, aliliambia MTANZANIA jana kuwa mpaka sasa wamezipata taarifa hizo kupitia magazeti tu na hakuna barua yoyote iliyofika kwao kutoka Yanga ikionyesha kuwa wanamuhitaji Kipre Tchetche.

“Hakuna barua yoyote tuliyopokea kutoka Yanga kama inavyodaiwa, Kipre Tchetche bado ni mchezaji wetu, ana furaha kuwa hapa, ana mkataba mrefu Azam FC na bado ataendelea kuwa hapa.

“Imekuwa ni kawaida sana kutokea hali hii kila usajili unapofunguliwa, hivi sasa wachezaji wetu wapo mapumzikoni na hatutaki wasumbuliwe,” alisema.

Mpaka sasa ligi ikiwa imesimama, Azam FC ndiyo vinara wakiwa na pointi 25 kwenye msimamo, wakifuatiwa na Yanga iliyojikusanyia pointi 23, Mtibwa Sugar 22 na Simba 21.RE

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles