30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Azam ‘yaikokia bunduki’ Mbeya City

Theresia Gasper-Dar es salaam

BAADA ya kulazimisha sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar juzi, kikosi cha Azam kimeelekea mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa Jumapili Uwanja wa Samora mjini humo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jafar Idd, alisema wameifuata Mbeya City a wakiwa na morali ya juu ya kuzitaka pointi tatu, baada ya mchezo wa juzi kutoka sare.

“Baada ya mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar tumeondoka leo (jana) kwenda Iringa, ambako   tutacheza mchezo wetu na Mbeya City, kwani mipango yetu ni kuvuna pointi tatu muhimu,” alisema.

Alisema wanatarajia mchezo dhidi ya Mbeya City utakuwa na ushindani mkubwa, lakini wamejipanga kupata ushindi na kupanda juu ya msimamo wa ligi hiyo.

“ Kwa ujumla hali ya kikosi ni nzuri wachezaji wote walioenda Iringa wapo fiti hakuna majeruhi zaidi ya Shaban Chilunda ambaye tumemuacha kutokana na kutumikia kadi nyekundu,”alisema Idd.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles